ASANTE MAMA
"Mwanangu soma kwa bidii uwe na maisha mema"
Hayo ni maneno niliyoambiwa na mamangu nikiwa mchanga
Nayakumbuka wa leo ilhali sikuambiwa jana
Bado yanarun so fresh kwa mind ni kweli yamenibana
Niliyatilia maanani hadi wa leo yananiongoza
Najikaza sana nipambane na hali angalau nitoboe hii maisha
Daily kushoto kulia sikosi pressure
Lakini namtegema Mola ndio yote niweze kuepuka
In my prayers lazima nimkumbuke wangu mama
Alinionesha njia life yangu ikawa ya maana
Kila Jumapili kanisani alifanya nikatangulia
Mfukoni alihakikisha sikukosa sadaka
Ata kama ingekuwa ni shilingi moja
Bora nimestretch mkono kwa kikapu nishukuru Maulana
Tulishinda njaa mchana kutwa na jioni pia tungelala tumbo kavu
Hatungeafford angalau mkate kavu
Lakini yote tisa kumi lazima tungeshukuru
Asante mama kwa kunifunza mema na mabaya
Ukaniambia kuna heaven na kunayo hell
Ningekosea kiboko lazima ingeland kwa yangu body
Liwe kosa ndogo ama kubwa,ulinifunza kosa ni kosa
Shuleni pia mwalimu alinifunza maadili
Kuhesabu moja,mbili,tatu hadi kumi
Akanifunza kutegua vitendawili na kutumia methali
Shukrani kwa mama sababu angetaka angekaa nami nyumbani
Elimu ndio taa
Tia bidii ndio uweze kung'aa
Shuleni waliniambia
Ndio utimize ndoto zako za kupaa
Lakini si pia talanta husaidia?
Hilo hawakuniambia
Ila nilikuja gundua
Shukran sana to the one above
Mahali nimefika ni yako favour
Kila ninacho ni wewe umenipa
©Crucial
Aaaaawwww
ReplyDeleteAsante Mama
Thumb up Crucial
Keep it up girl.
ReplyDeleteYou are going far.
Keep it up girl.
ReplyDeleteYou are going far.