Mimi si preacher
but napreache peace
mimi si athlete
but naipeleka adi kwa race
sisi sote ni wakenya
kukushow hivyo sitahesitate
damu yako na yangu twaweza ipaste
ndani yetu red ndio flow
so ata tushikane,there'll be no shock
koz tunaryme ki blood flow
usiangalie skin colour,sisi sote rangi ya thao
uwe dark ama bright
usimind,kuna waliobleach
Jan-Dec tuko na wewe huko beach
lakini mbona Siku flani ifike unigeukie
mkuki unitie
bullet utumilie kwa yangu heart
petrol umebeba ukachome yangu hut
utani tena kati yetu hakuna,it hurts
just because MTU WAKO alikulipa punch
akakushow enda huko,face zao uzipunch
na yeye akabaki kwake akirelax
remote mkononi breaking news akiwatch
shule ya mtoi wako umetia kiberiti
church yako mtaani ukamwagia petroli
mawe ukatupia nyumba ya jirani
haya yote MTU WAKO anawoch kwa teli
after a week ndio utarealise ulitumiwa
koz marafiki hunao tena
ulishawatafuna kama miwa
mama mboga kumbe alienda?koz ulichoma yake kibanda
mwenye duka hayuko pia,oh! kumbe biashara yake ulivamia
umebaki mwenyewe 'kijililia
MTU WAKO tena hapatikani,hafiki tena mashinani
alishatumia yako imani
sasa umebaki ukimlaumu nani??
cc Crucial